Maajabu ya pacha kufariki siku moja

Maajabu ya pacha kufariki siku moja

NA KITAVI MUTUA

NDUGU wawili pacha, Onesmus Susa Mati na Gabriel Mutie Mati, waliozaliwa siku moja, wamefariki siku moja katika kisa ambacho kimeshangaza familia zao na majirani.

Ndugu hao walikuwa marafiki wa kufa kuzikana tangu utotoni mwao, wakiwa shuleni na hatimaye wakajenga wakiwa majirani katika kijiji cha Mangina, wilaya ya Katulani, Kaunti ya Kitui.

Katika miaka 63 walioishi, familia zao na majirani walizoea hali kwamba walifanana kisura na kitabia lakini hawakutarajiwa kuwa wangefariki siku moja.

“Tumeshangazwa na vifo vyao vya ghafla. Lakini kama familia tumeshangazwa na mpango wa Mungu kwa kuchukua mioyo yao siku moja wakitofautiana kwa masaa matano pekee,” akasema Bi Kalau Susa, binti ya Onesmus.

Alieleza kuwa babake amekuwa akiugua tangu Jumatano wiki iliyopita na akalazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kitui.Siku iliyofuata, ndugu yake Gabriel aliamka mapema na kuelekea hospitalini kumjulia hali ambapo alikaa na nduguye hospitalini mchana kutwa.

Kulingana na Bi Kalau, ndugu hao wawili walizungumza kwa muda mrefu na hata wakashiriki chakula katika wadi ya hospitali.Lakini familia zao hazikufahamu kuwa hiyo ndio ilikuwa siku yao ya mwisho duniani.

“Gabriel alipofika nyumbani aligua ghafla usiku na kuaga tulipokuwa tukijiandaa kumkimbiza hospitalini, akaseme mkewe, Florence MuteiNaye Onesmus alifariki masaa matano baadaye alipokuwa akihamishwa kupelekwa hospitali ya Nairobi Womens jijini Nairobi.”

“Licha ya kuwa hakujua nduguye amekufa, baba alikuwa akisema alikuwa njiani kuungana na Gabriel,” akasema bintiye Onesmus.

 

You can share this post!

Kalonzo amponda Ruto kwa kupinga wazo la urais wa mzunguko

Polisi wengi wagura kazi, walia wanalipwa mshahara wa kitoto