Maandamano yaendelea Chad wiki kadhaa baada ya kifo cha Idriss Deby

Maandamano yaendelea Chad wiki kadhaa baada ya kifo cha Idriss Deby

Na MASHIRIKA

N’DJAMENA, CHAD

POLISI katika jiji kuu la Chad, N’Djamena, Jumamosi walifyatua vitoa machozi kuwatawanya makundi ya waandamanaji waliokuwa wakipinga hatua ya wanajeshi kutwa uongozi wa nchi.

Hii ni baada ya kifo cha Rais wa miaka mingi Idriss Deby katika uwanja wa vita kaskazini mwa nchi hiyo.

Serikali ya mpito, inayoongozwa na mwanawe Deby, Jenerali Mahamat Idriss Deby, Ijumaa ilipiga marufuku maandamano yote yaliyokuwa wakiendeshwa na vyama vya upinzani na makundi ya mashirika ya kijamii.

Makundi hayo yanataka serikali ya mpito inayoongozwa na kiongozi raia.

Jumamosi wanachama wa makundi hayo walikaidi marufuku hayo na kufurika barabarani wakitoa kauli zao na kupeperusha vijibendera. Wengine walibeba mabango yenye jumbe zinazokashifu kile walichotaja kama “ufalme.”

Polisi walitumia vitoa machozi kutawanya mikutano katika mtaa mmoja kusini mwa N’Djamena, wanahabari waliripoti.

“Polisi walituzuia kufanya maandamano,” Real Mianrounga, kiongozi wa kundi moja la kijamii, alinukuliwa akisema.

Aliongeza kuwa alijeruhiwa alipokuwa akitoroka polisi walipovunja mkutano wao eneo la kati mwa N’Djamena.

“Wale waliopinga walishambuliwa kikatili na polisi. Baadhi ya watu waliumia,” Mianrounga akaongeza.

You can share this post!

Real, Barcelona na Juventus watetea kuhusika kwao kwenye...

Bayern Munich watia kapuni taji la Bundesliga kwa mara ya...