Mabadiliko ya makamanda wa polisi yafanyika Makadara

Mabadiliko ya makamanda wa polisi yafanyika Makadara

Na SAMMY KIMATU

MABADILIKO ya uhamisho mkubwa wa maafisa wa polisi yamefanywa katika kaunti ndogo ya Makadara, Nairobi.

Mkuu wa eneo hilo kwa wakati huu ni Bw Matthew Gwiyo ambaye anachukua nafasi ya Bw Abdikadir Sheikh Ahmed ambaye amestaafu.

Naibu wa Bw Gwiyo ni Bi Judith Nyongesa huku Afisa anayesimamia Operesheni katika eneo hilo akiwa ni Bi Lydia Parteiyie.

Kabla ya uhamisho wake, Bw Gwiyo alihudumu katika cheo hicho katika kaunti ndogo ya Mbooni.

Kamanda mpya wa kituo cha polisi cha Industrial Area ni Bw Festus Maingi ambaye alichukua nafasi kutoka kwa Bw Amos Shamalla.

Bw Shamalla alihamishiwa hadi kituo cha Polisi cha Ongata Rongai.

Kamanda wa kituo cha polisi cha Makongeni ni Bw Stanley Mbuvi.

Akiongea jana, Bw Gwiyo alisema mabadiliko hayo ni ‘uhamisho wa kawaida’ uliokusudiwa kuongeza ufanisi katika huduma ya polisi.

“Baada ya kila miaka mitatu, maafisa huhamishwa kuhudumu katika maeneo mengine ya nchi kama sera ya polisi,” Bw Gwiyo alisema.

Mabadiliko mengine yalifanywa katika kambio mbalimbali pia.

Sajini David Chirchir anachukua nafasi ya kamanda wa polisi katika kambi ya Hazina.

Bw Chirchir alichukua nafasi kutoka kwa Inspekta John Odaro.

Afisa anayesimamia kambi ya Commercial ni Coplo John Nyaweya wakati kamanda wa Mariguini ni Inspekta Daniel Letting,

Katika kambi ya polisi eneo la Lunga Lunga, kamanda ni Inspekta Osman Hassan.

Katika Landi Mawe, inspekta Adan Abdi ndiye anayesimamia kambi hilo huku katika kambi ya Balozi kamanda ni Inspekta Robert Oberi.

Vilevile, Inspekta Humphrey Kinoti aliwekwa kuwa msimamizi wa kambi ya Kaloleni huku katika eneo la Reuben post afisa anayesimamia ni inspekta Abdirazak Sama.

Bw Gwiyo aliwaomba wananchi washirikiane na maafisa hao kumaliza uhalifu katika maeneo husika.

‘’Maafisa wangu wana ujuzi na weledi kwa kazi kwani wapepata mafunzo kutoka vyuo vyetu vya polisi,’’ Bw Gwiyo asema.

You can share this post!

Shirika la The Voice Kiambu lafadhili watoto mayatima

Pep aridhishwa na rekodi ya Man-City kwenye vita vya...