Habari Mseto

Mabapa mapya ya magari yaanza kutolewa

November 19th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

MAMLAKA ya Uchukuzi na Usalama (NTSA) imetangaza kuwa serikali imeanza kutengeneza upya nambari za usajili wa magari.

Katika taarifa, mkurugenzi mkuu wa NTSA Francis Meja alisema upungufu au ukosefu wa mabapa ya usajili ya magari ulisababishwa na ukosefu wa malighafi.

“Suala hilo limesuluhishw ana hivi sasa utengenezaji wa mabapa umeanza tena,” alisema katika taarifa.

Kutokana na hali, msururu mkubwa wa Wakenya wamekuwa wakingoja kupata mabapa ya usajili ya magari yao.

Walionunua magari nje ya nchi bado wanangoja kwani magari hayo hayawezi kuachiliwa forodhani bila nambari za usajili.

NTSA ilisema kuwa inajitahidi kutoa leseni bila kuchelewa kwa wamiliki wa magari ili yaweze kuachiliwa bandarini.