Habari MsetoSiasa

Mabwanyenye wote walipe ushuru wa juu – Uhuru

November 1st, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Rais Uhuru Kenyatta anataka Mamlaka ya Kukusanya Ushuru (KRA) kulazimisha matajiri kufichua kiini cha mali yao kwa lengo la kujua jinsi nzuri ya kutoza ushuru.

“Wanaoishi maisha ambayo hayaambatani na ushuru wanaolipa wanafaa kulazimishwa kufichua kiini chao cha mali,” alisema Rais wakati wa kuzindua mfumo mpya wa kusimamia ulipaji ushuru KRA.

Kulingana na rais, kulenga matajiri kutawezesha KRA kuimarisha mapato na kukuza idadi ya walipaji ushuru.

Kulingana na rais, idadi ya wananchi ambao hulipa ushuru bado iko chini sana hali inayowafanya wanaolipa ushuru kulemewa na mzigo mkubwa wa ushuru.

Awali, Waziri wa Fedha alikuwa amependekeza ushuru wa asilimia 35 kwa wote ambao hulipwa Sh750, 000 na zaidi kwa mwezi.Hata hivyo, baadaye aligeuza msimamo huo baada ya kupata maoni ya Wakenya.