Macho kwa Neymar timu ya Brazil ikiendea Ghana kirafiki leo

Macho kwa Neymar timu ya Brazil ikiendea Ghana kirafiki leo

NA MASHIRIKA

LE HARVE, Ufaransa

HUKU Brazil ikipangwa kumenyana na Cameroon kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar mnamo Desemba 2, miamba hao wameamua kujipima nguvu dhidi ya Ghana ugani Ocean, Ufaransa leo Ijumaa na Tunisia hapo Septemba 27.

Brazil hawajakung’utwa tangu wapoteze taji la Copa America dhidi ya Argentina mnamo Julai 2021.

Wameshinda mara 10 na kutoka sare mechi tatu italazimika kufanya kazi ya ziada kufuta historia duni dhidi ya Wabrazil. Ghana imepoteza mechi zote nne dhidi ya Brazil bila kufunga bao katika tatu.

Macho yatakuwa kwa mshambulizi Neymar (Paris Saint-Germain) na kiungo Mohammed Kudus (Ajax Amsterdam).

Ghana ya kocha Otto Addo huenda ikachezesha mzawa wa Uhispania Inaki Williams aliyeamua kuwakilisha taifa ambalo wazazi wake walitoka.

Ratiba

(Septemba 23): Korea Kusini v Costa Rica (2.00pm), Cameroon v Uzbekistan (3.00pm), DR Congo v Burkina Faso (3.00pm), Misri v Niger (3.00pm), Japan v Amerika (3.25pm), Canada v Qatar (6.00pm), Bahrain v Cape Verde (7.00pm), Uruguay v Iran (7.00pm), Paraguay v UAE (8.00pm), Saudi Arabia v Ecuador (9.00pm), Brazil v Ghana (9.30pm), Algeria v Guinea (10.00pm), Mali v Zambia (10.00pm), Morocco v Chile (10.00pm).

  • Tags

You can share this post!

Arror, Kimwarer: Mashahidi sasa walia kutishwa

MAWAIDHA YA KIISLAMU: Dunia ya leo yahitaji dua kwa wingi...

T L