Macho yote yaelekezwa Bomas Wakenya wakisubiri kwa hamu kujua atakayekuwa Rais wa Tano

Macho yote yaelekezwa Bomas Wakenya wakisubiri kwa hamu kujua atakayekuwa Rais wa Tano

NA SAMMY WAWERU

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inasubiriwa kutangaza leo Jumatatu saa tisa matokeo ya kura za kiti cha urais zikiwa ni siku sita baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.

Chini ya muda wa siku tano, tume hiyo imekuwa ikithibitisha fomu 34A na 34B katika ukumbi wa Bomas of Kenya, jijini Nairobi.

Tayari shughuli ya kujumlisha imekalika, na imeashiria matokeo yanaweza kutangazwa.

IEBC aidha imetuma mwaliko kwa vyombo vya habari kupeperusha tangazo hilo, wakati mwenyekiti wake, Bw Wafula Chebukati atakuwa akitoa matokeo.

Imeratibu saa tisa alasiri kama wakati rasmi kutangaza atakayekuwa Rais wa tano, Jamhuri ya Kenya.

Wadhifa huo uliwaniwa na wagombea wanne: Raila Odinga (Azimio), William Ruto (Kenya Kwanza), George Wajackoyah (Roots Party) na David Mwaure wa Agano Party.

  • Tags

You can share this post!

MWALIMU WA WIKI: Mwalimu stadi, mbunifu kazini

Mbunge wa zamani afaulu udiwani Wadi ya Jaribuni

T L