Habari za Kitaifa

Mackenzie arudishwa kortini kukabiliwa na mashtaka ya vifo vya watoto 191

February 6th, 2024 1 min read

NA ALEX KALAMA

MHUBIRI tata Paul Mackenzie anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji yaliyotokea msituni Shakahola amewasili katika Mahakama Kuu ya mji wa Malindi ili yeye na wenzake zaidi ya 30 kukabiliwa na mashtaka 191 ya vifo vya watoto 191.

Hii ni baada ya muda wa kuenda kufanyiwa uchunguzi wa akili kukamilika.

Tayari serikali imetangaza kwamba kanisa lake la Good News International ni kundi la uhalifu.

Soma Pia: Kanisa la Mackenzie ni kundi la uhalifu – Serikali

Mbali na Bw Mackenzie, pia kuna Mary Kahindi ambaye ni mke wake Smart Mwakalama Deri.

Bi Kahindi ni miongoni mwa hao washukiwa 30.

Bi Mary Kahindi, ambaye ni mke wake Bw Smart Mwakalama Deri, ashuka kutoka kwa gari la kuwabeba mahabusu na wafungwa. PICHA | ALEX KALAMA

Inadaiwa kwamba Bw Mwakalama ndiye alikuwa msaidizi mkuu wa shughuli za kidini zilizoongozwa na Bw Mackenzie.

Polisi wamekuwa wakichunguza kundi la mhubiri huyo kwamba liliwapa waumini mafunzo potovu yaliyosababisha wao kufunga hadi kufa kwa kuaminishwa kwamba wangekutana na Yesu.