Habari Mseto

Mademu wa Kenya ni moto chumbani – Diamond Platnumz

January 4th, 2019 1 min read

NA THOMAS MATIKO 

NYOTA wa Bongo Flava Diamond Platnumz kadai kuwa mademu wa Kenya ni wakali kwenye mchezo wa kitandani na ndio sababu mastaa wa kibongo wanavuka boda.

Staa huyo ambaye kwa sasa anatoka na kichuna Mkenya mtangazaji wa radio ya NRG, alitoa kauli hiyo kwenye shoo yake ya Wasafi Festival iliyofanyika Uhuru Gardens kuukaribisha mwaka mpya.

Baada ya kutumbuiza kwa muda, Diamond alisita kidogo na kuanza kupiga stori na mashabiki wake. “Halafu Kenya niwaambie kitu, mna watoto wazuri sana. Ni warembo, wana heshima na kwenye michezo ya kitandani ni mafundi sanaa. Ndio maana mastaa wabongo tunakimbia kuwafuata watoto Kenya,” alidai.

Ukiachana na yeye, yupo pia staa AliKiba ambaye baada ya kuwa kwenye mahusiano na vichuna wengi wa kibongo ikiwemo Jokate Mwengelo, aliamua kuja Kenya na kumwoa kichuna Amina Khalef kutoka Mombasa.

Vile vile kwa sasa staa mwingine wa Bongo Ben Pol anatoka kimapenzi na kichuna mfanyibiashara mtajika Anerlisa Mungai.