Habari Mseto

Madiwani wa Jubilee waitwa kwa mkutano wa chama

August 13th, 2020 1 min read

 COLLINS OMULO na FAUSTINE NGILA

Chama cha Jubilee kimewaita madiwani wake wa bunge la Nairobi kwenye mkutano wa dharura jioni ya Alhamisi.

Hii inajiri mbele ya kuchaguliwa kwa spika mpya Ijumaa baada ya kujiuzulu kwa Beatrice Elachi Jumatano.

Mkutano huo ambao umeitwa na katibu mkuu wa chama hicho utaandaliwa kwenye makao makuu ya chama hicho.

“Kuhusiana na maendeleo ya hivi karibuni ya bunge ya kaunti ya Nairobi unatakikana kuhudhuria mkutano wa ushauri , mnahitajika kuhudhuria mkutano madiwani waliochaguliwa na kuteuliwa kwenye makao makuu ya Jubilee Pangani saa sita Agosti 13, 2020 bila kuchelewa,” ilisoma barua ya Bw Tuju.

Chama hicho cha Jubilee kina madiwani 65 wa kuchanguliwa na kuteuliwa baada ya diwani mteuliwa Habiba Hussein alipoteza nafasi yake baada ya kukosa kikao cha bunge kwa miaka miwili.