Habari MsetoSiasa

Madiwani wa Jubilee waitwa na Tuju ofisini

June 8th, 2020 1 min read

NA COLLINS OMULO

Madiwani waliochaguliwa kupitia tiketi ya chama cha Jubilee wameitwa na viongozi wakuu wa chama hicho huku kukishuhudiwa na hali za sintofahamu katika bunge la Kaunti ya Nairobi.

Katibu mkuu wa cham cha Jubilee Raphel Tuju ameita mkutano wa dharura kwa madiwani wote Jumatano katika makao makuu ya chama hicho eneo la Pangani.

Katika barua iliyotolewa na Bw Tuju, mkutano huo utaanza saa tano kamili na utajadili masuala ya chama hicho.

“Hii ni kuwaomba mhudhurie mkutano katika makao makuu ya chama na tafadhali mtilie maanani mkutano huu na mfike bila kuchelewa,” alisema Bw Tuju katika barua hio ya Juni 8.

Mkutano huo ulikuwa ufanyike Jumanne lakini Bw Tuju akaupeleka Jumatano Juni 10, 2020.