Habari Mseto

Madiwani Wajir mbioni kumtimua gavana

August 20th, 2020 1 min read

BRUHAN MAKONG NA FAUSTINE NGILA

Madiwani wa Kaunti ya Wajir wamepeana notisi ya kumng’oa mamlakani gavana wa kaunti hiyo Mohamed Abdi kwa madai ya ufisadi na matumizi mabaya ya afisi.

Notisi hiyo ilitolewa na diwani wa wadi ya Abdi Mhamed Sheikh aliyemuomba karani wa kaunti hiyo kuharakisha shughuli hyio.

Hayo yanajiri baada ya mazungumzo baina ya wazee, viongozi wa kisiasa na madiwani.

Bw Sheikh na madiwani wenzake wanaamini kwamba gavana huyo ametumia vibaya mamlaka yake na kwenda kinyume na katiba. Alisema kwamba mswada huo wa kumtoa malakani umezingatia amri za kisheria.

Aliwaomba wananchi wa Wajir waunge mkono mchakato huo. “Tunaomba kuungwa mkono na wananchi wa Wajir huku tukiketeleza haya,”alisema.

Diwani huyo wa Bute alisema kwamba ni kazi ya afisi ya karani kuwasilisisha mswada kwa spika ambaye atauwakilisha kwa kamati ya bunge hilo ili uangaziwe.