Habari

Madiwani wapitisha hoja ya kumbandua Waiguru

June 9th, 2020 1 min read

Na GEORGE MUNENE

MADIWANI wa Kirinyaga wapitisha hoja ya kumbandua Gavana Anne Waiguru baada ya kikao cha kujadili hoja hiyo iliyowasilishwa na Kinyua Wangui ambaye ni diwani wa wadi ya Mutira.

Takriban madiwani 23 kati ya 33 wameunga mkono hoja hiyo iliyojadiliwa kuanzia Jumanne asubuhi.

Waiguru anaelekezewa lawama kwamba anatumia mamlaka yake vibaya na kwamba pia anahusika katika ufisadi.

Vurumai zimeshuhudiwa asubuhi madiwani kadhaa waliporushiana makonde wakati wa kujadiliwa hoja hiyo.

Waiguru hata hivyo amejitetea akisema kwamba hoja hiyo inakiuka agizo la mahakama.