Mafunzo ya marefarii wa Ligi ya Taifa Divisheni ya Kwanza kukamilika leo Jumatano

Mafunzo ya marefarii wa Ligi ya Taifa Divisheni ya Kwanza kukamilika leo Jumatano

Na AREGE RUTH

MAFUNZO ya waamuzi wa mechi za Ligi ya Taifa ya Divisheni ya Kwanza, yanakamilika leo Jumatano katika uga wa kimataifa wa Kasarani mjini Nairobi.

Makamu wa Rais wa Shirikisho la soka nchini (FKF) Doris Petra, Jumatatu, Novemba 28, 2022, aliongoza hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo ya lazima ya siku tatu kwa maandalizi ya msimu mpya.

Wasimamizi 200 wa mechi walifanya mazoezi mepesi uwanjani kuthamini wepesi wao wa kimwili. Pia, walifanyiwa vipimo vya afya vya ambavyo vilitathmini utimamu wao wa kusimamia mechi za ligi.

Hapo jana, walifanya mafunzo mengine darasani kupitia madarasa ya uadilifu na pia marekebisho ya sheria za mchezo msimu wa mwaka 2022/23 kupitia kwa Mkuu wa Uadilifu wa Shirikisho la Soka nchini (FKF) Mike Kamure.

Mafunzo hayo yaliongozwa na waamuzi wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Margaret Omondi, Stephen Oduor, Tabitha Wanjiru, Dorcas Moraa, Moses Osano, na Damaris Kimani.

Ligi hiyo ya wanawake na wanaume inatarajiwa kuanza tarehe 10 mwezi ujao.

 Kwa upande mwingine, idara ya Mashindano ya ligi ya FKF ilifunga sajili ya wachezaji wa nje na ndani ya Kenya. Dirisha hilo lilifungwa rasmi tarehe 28 mwezi huu.

Ligi zote mbili za FKF za wanawaume tayari zimeanza. Ligi ya Kuu ya Wanawake (KWPL) inatarajiwa kung’oa nanga wikendi hii.

You can share this post!

Wachungaji Thika wawatolea wito Wakenya waiunge mkono...

Maandamano: Raila akunja mkia

T L