Habari Mseto

Mafuriko yasababisha shule 5 kuhamisha wanafunzi

October 16th, 2020 1 min read

NA SHABAN MAKOKHA

Shule tano kaunti ya Busia zimebakia kufungwa kwa sababu ya mafuriko. Kwenye eneobunge la Budalangi shule za Rugunga, Buongo, Musomana Igigo zimesalia kufungwa.

Mto Nzoia ulivunja kingo chake huku maelfu ya watu wakikipoteza makao na kuharibu vitu vya thamani ambayo haijulikani.

Mkurugenzi wa masomo kutoka Magharibi wa Kenya Stephen Baarongo alisema kwamba wanafunzi kutoka maeneo yalioathirika watalazimika kutafuta shule kwingine.

Wanafunzi waa shule ya Igigo wamepelekwa shule ya Budalangi huku wa Musoma wakipelekwa shule ya Rugunga..

Wanafunzi wa Rugunga wamepelekwa Lugale huku wanafunzi wa Buongo wakipelekwa Mubwayo.Wale wa Musoma kwa sasa wanasomea chuo cha kufunza walimu cha Sango.

Bw Barongo alithibitisha kwamba shule zenye ziko eneo hilo zilizotumika kama maeneo ya maficho kwa waliohadhirika na mafuriko ziko salama  kwa wanafunzi kwani zilinyunyuziwa dawa.

BMwakilishi wa wanawake Florence Mutua aliomba serikali kutengeneza shule  hizo kabla ya wanafunzi kurudi shuleni.

“Tunataka wanafunzi kutoka maeneo yalioathirika wasaidiwe ili warudi kusoma.Vyoo vimenjaa maji na hii inaweka Maisha ya wanafunzi hatarini ya kupata  magonjwa kama Cholera na Bilrhazia,”alisema Bi Mutua.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA