Habari Mseto

Mafuta ya kupikia yaliyoharibika 2018 yanaswa Mombasa

June 14th, 2020 1 min read

MOHAMED AHMED

Maafisa wa kitengo cha Upelelezi wa Jinai [DCI] walinasa lita 25,300 za mafuta ya kupikia ambayo siku zake za kutumiwa zilikuwa zimepita, Kaunti ya Mombasa.

Maafisa hao walinasa mafuta hayo yaliyopakiwa kwenye mitungi ya lita 20 katika eneo la Denco Changamwe.

Mafuta hayo yalikuwa yanapakiwa ili yauziwe wakazi licha ya mwenyewe kujua kwamba mafuta hayo yalikuwa yameharibika.

Mafuta hayo yaliyotenenezwa Desemba 2017 yaliharibika Desemba 2018 .DCI kupitia mtandao wa Twitter iliripoti kwamba mmiliki anajulikana kam Bi Deborah Taabu.

“DCI iliwaonya wanaosambaza chakula kilichoharikiba kwa sababu ya tamaa ya pesa watakamtwa,” ulisoma ujumbe huo.

Mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Changamwe.