Habari za Kitaifa

Mafuta yashuka kwa Sh1 mwezi mmoja baada ya kuteremka kwa hadi Sh18

May 14th, 2024 1 min read

NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Kudhibiti Kawi Nchini (EPRA) imetangaza bei mpya za mafuta ambapo kwa wastani, kuna kushuka kwa kati ya Sh1 na Sh1.30.

Katika bei hizo mpya, mafuta ya petroli yameshuka kwa Sh1 hivyo basi lita moja Nairobi itauzwa Sh192.84 huku dizeli ikishuka kwa Sh1.20 na kufanya bei kuwa Sh179.18 nayo mafutataa yakipungua kwa Sh1.30 na kusababisha yauzwe kwa Sh168.76 kwa lita.

Kushuka huko ni kudogo mno ikilinganishwa na mwezi jana ambapo mafuta yalishuka kwa hadi Sh18.68 (mafutataa), Sh10 dizeli na 5.31 na kuoneka kuwa afueni kubwa kwa Wakenya wanaopambana na hali ngumu ya uchumi pamoja na gharama kubwa ya maisha.