Habari Mseto

Magelo ataka maduka ya Ngong yasipeanwe

September 15th, 2020 1 min read

Na Collins Omulo

Aliyekuwa spika wa Kaunti ya Nairobi Alex Ole Magelo ameomba serikali kuu kusitisha kupeanwa kwa maduka 1,653 ya kufanyia biashara kwenye soko la Ngong.

Alitaja kwamba wafanyabiashara wengi wameachwa kwenye mpango huo wa kuepa na maduka na wanafanyia kazi kwenye soko mze ya Ngong.

Kulingana na Bw Ole Magelo wafanyabiashara wengi waliopata mgao wa maduka hayo si wa kutoka mji wa Ngong au kaunti ya Kajiado.

“Naunga mkono serikali kuu lakini kwa hili naeza pendekeza wasitishe mgao wa maduka hayo.Kwani huwezi toa wafanyabiasghara nje ya kaunti  na kuwapa nafasi kwenye soko huku wenyeji wakikosa,”alisema Bw Maagelo.

Alisema kwamba mgao huyo umefanyika kinyume na wakazi ambao walikosa mgao huyo.

Tafsiri na Faustine Ngila