Habari

Magoha aitaka Knec kuweka wazi mada zitakazotahiniwa kwenye mtihani wa Gredi ya Tatu

August 1st, 2019 1 min read

Na WANDERI KAMAU

WAZIRI wa Elimu Prof George Magoha ameagiza Baraza la Kitaifa la Mitihani (Knec) kuweka wazi masuala na mada ambazo zitatahiniwa kwenye mtihani wa Gredi ya Tatu unaotarajiwa Septemba.

Akihutubu katika kongamano maalumu kuhusu hatua zilizopigwa katika mfumo mpya wa elimu – unaojikita kwa umilisi – katika Gredi ya Tatu, waziri amesema hatua hiyo itaondoa taharuki iliyopo miongoni mwa wazazi na wadau wa elimu kuhusu mtihani huo.

“Mtihani huo haupaswi kuzua wasiwasi miongoni mwa wanafunzi kwani watatahiniwa kuhusu masuala waliyofunzwa,” amesema Magoha.