Magoha asisitiza sharti kiboko kirejee shuleni

Magoha asisitiza sharti kiboko kirejee shuleni

Na WYCLIFFE NYABERI

WAZIRI wa Elimu, George Magoha amerejelea kampeni yake ya kutaka kiboko kirudishwe shuleni.

Prof Magoha alisema yeye binafsi hangefika mahali aliko kimaisha ikiwa wazazi na walimu wangekosa kumwadhibu kwa kumcharaza kiboko.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Shule ya Msingi ya Egetonto, eneobunge la Mugirango Kusini, Kaunti ya Kisii madarasa mapya yaliyojengwa na wataalamu wa jamii ya Abagusii wanaohudumu serikalini, Prof Magoha alisema utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi nchini umechangiwa zaidi na wao kukosa kuadhibiwa wanapokosa.

Madarasa hayo matano ya kisasa, yalijengwa baada ya masaibu ya wanafunzi wa shule hiyo kuangaziwa na vyombo vya habari wakisomea ndani ya nyumba za tope.Naye Waziri wa Usalama, Fred Matiang’i kwa alisema wakati umefika sasa kwa taifa kuandaa mdahalo wa namna linaweza kukabili tatizo la utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi.

Dkt Matiang’i alisema serikali na wazazi hutumia pesa nyingi kugharamia hasara kubwa inayosababishwa na wanafunzi wanapojihusisha kwenye uchomaji wa mabweni, jambo alilosema haliwezi likakubalika kuendeleaWaziri Magoha pia alieleza kuwa mitihani ya kitaifa ya 2021 itakayofanywa Machi mwaka ujao imekamilika kuandaliwa, akiwahakikishia watahiniwa kuwa wametilia maanani matatizo yaliyosababishwa na Covid-19.

You can share this post!

Matusi dhidi ya Raila yamwandama Uhuru

Ruto akausha mahasla kwa kukosa kuwasili kuwachangishia pesa

T L