Magoha asogeza tarehe ya wanafunzi kurudi shuleni

Magoha asogeza tarehe ya wanafunzi kurudi shuleni

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Elimu Profesa George Magoha amesogeza mbele tarehe ya shule kufunguliwa kutoka Jumatatu, Agosti 15, 2022 hadi Alhamisi, Agosti 18, 2022.

“Kulikuwa na uchaguzi mkuu mnamo Jumanne, Agosti 9, 2022 na shughuli ya kujumlisha matokeo ya kura zilizopigwa inaendelea. Kwa hivyo, baada ya kufanya mashauriano ya kina, ninatangaza kwamba serikali imeahirisha tarehe ya kufunguliwa kwa shule za msingi na za upili kutoka Jumatatu, Agosti 15, 2022 hadi hadi Alhamisi, Agosti 18, 2022,” amesema waziri Magoha.

Ameongeza kusema kwamba ni agizo linaloanza kutekelezwa mara moja na kwamba lina uzito kuliko tangazo lolote la awali.

“Agizo hili ndilo la kuzingatiwa kwa sababu linawakilisha msimamo wa hivi punde kulinganisha na agizo lolote lililotolewa kabla ya hili,” amesema.

  • Tags

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Wakenya wachukulie kwa uzito mchakato wa...

Kioni: UDA ilichezea Jubilee rafu Mlimani

T L