Magoha kuzikwa Februari 11 kwake Gem

Magoha kuzikwa Februari 11 kwake Gem

NA KENYA NEWS AGENCY

ALIYEKUWA Waziri wa Elimu, Prof George Magoha atazikwa Februari 11, 2023, familia yake imesema.

Kulingana na kaka yake mkubwa, John Obare, Prof Magoha anayeheshimiwa kwa kupunguza udanyanyifu katika mitihani nchini, atazikwa katika boma lake Gem, Yala, Kaunti ya Siaya.

Akizungumza katika mazishi ya kaka yao mmoja marehemu, Prof Alex Nyabera Magoha Obare aliomba Wakenya kuombea familia kuhimili msiba wa kupoteza kaka wawili ndani ya wiki chache.

Obare na kaka yake mdogo, Joseph Ogle walipuuza hofu kuwa huenda kuna mtu aliyehusika katika vifo vya kaka zao.

Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Eugene Wamalwa aliyehutubia waombolezaji, alisema nchi imepoteza wana wenye bidii kwa vifo vya maprofesa hao wawili.

Katika siasa, Wamalwa alisema hakuna anayeweza kusimamisha Wakenya kujadili masuala yanayoathiri Wakenya.

Waziri huyo wa zamani aliyefanya kazi na Prof Magoha, alisema hatua ya viongozi wa Azimio kutaka serikali kuokoa Wakenya dhidi ya gharama ya juu ya maisha na kuzuia wizi wa kura hailengi kulazimisha Rais Ruto kugawana serikali na upinzani.

  • Tags

You can share this post!

Vihiga Queens wapigwa na Thika Queens katika KWPL huku...

Serikali kusaka wanaorai wasichana wa shule kushiriki...

T L