Habari Mseto

Magufuli afungua shule na shughuli zilizofungiwa

June 17th, 2020 1 min read

NA THE CITIZEN

Rais wa nchi ya Tanzania John Magufuli  ameamuru shule zifunguliwe hapo Juni 29.

Shule zilifungwa Machi kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa corona ambao umeathiri watu 5.1 milioni huku watu 333,000 wakifariki duniani .

Rais huyo alitangaza hayo alipohutubia bunge jijini Dodoma. “Kwasababu visa vya corona vimepungua humu nchini nachukua nafasi hii kutangaza kufunguliwa wa shule zilizobaki, na shughuli zingine ambazo zilifungiwa kama harusi,’’ alisema.

“Maisha lazima yaendelee kama kawaida,’’ aliongeza.