Magufuli ampongeza waziri wa China kwa kutovaa maski

Magufuli ampongeza waziri wa China kwa kutovaa maski

NA MASHIRIKA

RAIS John Magufuli wa Tanzania amempongeza waziri kutoka China aliye ziarani nchini humo kwa kutovaa barakoa, akidai hilo ni ithibati tosha virusi vya corona havipo katika taifa hilo.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa China, Wang Yi, yuko kwenye ziara ya kikazi nchini humo.

“Ningetaka kumshukuru Waziri Wang Yi kwani kwani anajua Tanzania hakuna corona. Hiyo ndiyo sababu hajavaa barakoa. Ahsante sana. Ili kuthibitisha hilo, nitamsalimia halafu baadaye tutashiriki kwenye chakula cha pamoja,” akasema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amekuwa akilaumiwa jinsi ambavyo amekuwa akishughulikia janga hilo, hasa kwa kupuuza masharti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu udhibiti wa maambukizi ya virusi hivyo.

Tanzania haijakuwa ikitoa maelezo kamili kuhusu hali ya maambukizi ya corona nchini humo.Waziri huyo yuko kwenye ziara katika nchi tano barani Afrika inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya taifa hilo na nchi za Afrika

.Nchi hizo ni Nigeria, DR Kongo, Botswana, Tanzania na Ushelisheli.

 

You can share this post!

Mawimbi ya BBI yanavyoyumbisha kundi la Kieleweke

Wanajeshi 23 waliofungwa kwa mauaji ya Kabila waachiliwa...