Habari Mseto

Mahabusu 5 waliohepa jela wasakwa Meru

August 16th, 2020 1 min read

CHARLES WANYORO na FAUSTINE NGILA

Polisi eneo la Timau Kaunti ya Meru wanatafuta mahabusu watano waliohepa kutoka rumande Jumamosi usiku.

Walikuwa tayari washafikishwa kortini na kuwekwa rumande kwenye kituo cha polisi wakigoja kupimwa virusi vya corona kabla ya kupelekwa kwenye jela ya GK Meru.

Walihepa kupitia shimo waliochimba shimo kwenye ukuta ilionekana saa nne unusu usiku baada ya mahabusu wawili waliobaki walianza kupiga mlango huku kelekele hizo ikivutia konstebo wa Symour Symour Letta na Nelson Mwita .

Baada ya kutoka kwenye seli hio watano hao walikata ua na kutoroka.

Polisi walipata bibisi na waya zinaoaminika kutumika kuchimba shimo hilo. Washukiwa waliobaki walisema kwamba chuma yenye nguvu ilitumika kuchimba shimo hilo.

Kufuatia kutoroka kwa watano hao maafisa walitumwa kutafuta watano hao kutumia mbwa za usalama kutoka shamba la Lolmalik.

Waliohepa ni Debis Kaimenyi,aliyeshtakiwa kwa wizi,Silas Kinyua [wizi wa Magari],Daniel Murithi [Wizi wa Mifugo] Alvin Murithi [Unajisi] na Nicholas Kimathi

Mkuu wa polisi kaunti ya Meru Patrick Lumumba alisema kwamba hakuna mshukiwa aliyekamatwa na bado washukiwa hao wanendelea kutafutwa.