Habari Mseto

Mahabusu wawili waliotoroka wakamatwa

September 1st, 2020 1 min read

Na Hilary Kimuyu

Mahabusu wawili kati ya sita waliotoroka kwenye kituo cha polisi cha Kayole walikamatwa Jumatatu.

Kulingana na ujumbe wa polisi wawili hao, Dennis Ndung’u aliyezuiliwa kwa kosa la ubakaji na John Irungu alinaswa kwa makosa ya wizi wa mabavu walirudishwa ndani baada ya kukamatwa.

Polisi waliazisha msako wa kuwatafuta sita hao waliohepa kwenye njia isiyojulikana. Sita hao walihepa kupitia kwa paa.

Washukiwa wengine John Irungu, Tonny Makori, Francis Mwangi na John Mwangi wanaoshtakiwa kwa makosa ya wizi wa mabavu wanasubiri kupelekwa kufungwa Industrial Area.

Washukiwa wengine 11 walihepa kutoka kituo cha polisi cha Bungoma.

Kikundi hicho kilihepa kutoka kituo chaapolisi cha Bungoma ya kati baada ya kuchimba shimo usiku.Mshukiwa mmoja alikamatwa baada ya kupigwa risasi pajani alipokuwa akijaribu kuhepa.

Hii inajiri wiki moja baada ya mkuu wa polisi wa kituo cha polisi cha Bungoma Kusini Wilson Nanga kusema kwamba wengine wawili walihepa na kukamatwa tena.

“Maafisa wetu walikamata mshukiwa mmoja nyumbani kwake Manyanja Vitunguu .Pia tulikamata mshukiwa mwingine mji wa Webuye,”alisema Nanga.

Mkuu huyo wa polisi aliongeza kwamba mshukiwa aliyepigwa risasi alitibiwa kwenye kituo cha afya cha Bungoma na baadaye  akapelekwa kwenye kituo cha polisi cha Bungoma.

Tafsiri na Faustine Ngila