Koome aagiza mahakama zianze kusikiliza kesi kwa njia ya kawaida

Koome aagiza mahakama zianze kusikiliza kesi kwa njia ya kawaida

Na RICHARD MUNGUTI

JAJI Mkuu Martha Koome ameagiza mahakama kote nchini zianze kusikiliza kesi kwa njia ya kawaida kufuatia kuondolewa kwa sheria za kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona na Rais Uhuru Kenyatta.

Jaji Koome alisema kufuatia agizo hilo la Rais Kenyatta, inabidi mahakama zianze kusikiliza kesi hadharani badala ya kutumia mitandao.

Katika arifa iliyotolewa kwa majaji wote, mahakimu, kadhi mkuu na wanachama wote wa majopo ya kuamua mizozo, Jaji Koome alisema mahakama zinafunguliwa tena baada ya kupungua kwa maambukizi ya Covid-19.

Mahakama zilifungwa kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa virusi vya corona uliowaathiri majaji, mahakimu, makarani na wahudumu wengine katika idara ya mahakama.

Kufuatia kuzuka kwa ugonjwa huo, aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga na naibu wake Jaji Philemona Mwilu waliamuru mahakama zote zifungwe na kesi ziendeshwe kwa mitandao.

“Ili kuendelea kutoa huduma vyema zaidi, korti zote nchini zitaanza kutoa huduma kati ya saa tatu asuhubi hadi saa kumi na moja alasiri,” Jaji Koome aliagiza katika arifa aliyotoa.

You can share this post!

Serikali irejeshe spoti shuleni – Kuppet

Serikali yatangaza likizo fupi

T L