Habari Mseto

Mahakama mbili zafungwa kwa sababu ya corona

August 13th, 2020 1 min read

GEORGE MUNENE na FAUSTINE NGILA

Mahakama mbili kwenye kwenye Kaunti ya Kirinyanga zimefungwa Alhamisi baaada ya mwendesha mashtaka kupatikana na virusi vya corona.

Majengo hayo ya mahakama ya Wang’uru yatabakia kufungwa hadi Agosti 26, maafisa wa mahakama walitangaza.

“Najuta kuwaeleza kwamba mmoja wa waendesha mashtaka amepatikana na virusi vya corona. Kuhusiana na Wizara ya Afya wafanyakazi wa mahakama ya kwanza na pili watalazimika kujitenga,” Hakimu Mkuu G M Mutiso alisema kwenye ilani.

Kufuatia kufungwa kwa korti hiyo, wafanyakazi wote waliombwa wajitenge kwa siku 14.

Watapimwa virusi vya corona kabla ya kurudi kazini.