Mahakama ya Juu yatesa wabunge kwa kuzima CDF

Mahakama ya Juu yatesa wabunge kwa kuzima CDF

NA LEONARD ONYANGO

WAGOMBEAJI wa ubunge ambao wamekuwa wakitoa ahadi za kutekeleza miradi katika maeneo yao wamepata pigo baada ya Mahakama ya Juu kubatilisha Hazina ya Ustawishaji wa Maeneobunge (NG-CDF).

Majaji watano wakiongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome waliharamisha sheria ya CDF ya 2013.

Kila eneobunge hupokea Sh100 milioni kila mwaka kutoka kwa serikali kuu na hazina hizo hutumiwa na wabunge kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

Wabunge wamekuwa wakitumia fedha za NG-CDF kukarabati majengo ya madarasa, barabara na kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kutoka familia zisizojiweza.

Lakini Majaji Koome, Philomena Mwilu, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u na William Ouko walisema kuwa sheria hiyo inakinzana na Katiba.

Majaji hao wanasema majukumu ya wabunge ni kutunga sheria.

Hiyo inamaanisha wapigakura leo Jumanne wanahitajika kuchagua wabunge walio na uwezo wa kutetea masilahi yao Bungeni.

  • Tags

You can share this post!

Ruto apiga kura katika kituo cha Kosachei

Kipchoge afungua maktaba kwa umma Kapsisiywa

T L