Habari

Mahakama yakataa kuharamisha noti mpya

September 27th, 2019 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA Kuu imepuuzilia mbali kesi ya mwanaharakati Okiya Omtatah aliyowasilisha kupinga sura ya Hayati Mzee Jomo Kenyatta kwenye noti mpya, ikisema ni sehemu ya picha ya Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi.

Hii ina maana kwamba Mahakama imekataa kuharamiisha matumizi ya noti hizo mpya zilizozinduliwa Juni 2019 katika uwanja wa Narok na Gavana wa Benki kuu ya Kenya (CBK) Dkt Patrick Njoroge.

Noti ya Sh1000 ya zamani itapoteza thamani yake na kuacha kutumika ifikapo Septemba 30, 2019.

Tayari baadhi ya wafanyabiashara na hata mashirika yameanza kuikataa noti hiyo.