Mahakama yakataa kusitisha uchunguzi wa matamshi ya chuki

Mahakama yakataa kusitisha uchunguzi wa matamshi ya chuki

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA kuu imekataa kusitisha agizo la wanasiasa watatu kuchunguzwa kwa kueneza chuki.

Hata hivyo, Jaji Jairus Ngaah aliratibisha kuwa ya dharura kesi iliyoshtakiwa na vuguvugu la Sheria Mtaani na Shadrack Wamboi.

Kesi ya Sheria Mtaani inapinga agizo la Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IG) awachunguze kisha awashtaki Seneta Mithika Linturi (Meru), Mbunge wa Kitutu Chache Kusini Bw Richard Onyonka na Seneta wa Kericho Aaron Cheruiyot kwa kuchochea chuki cha kikabila.

Tayari Bw Linturi ameshtakiwa katika mahakama ya Nakuru kwa matamshi ya uchochezi akiwa Eldoret.

Katika kesi hiyo wakili Samuel Chelongo anasema masuala ya uchunguzi wa matamshi ya chuki ni jukumu la Tume ya Uwiano (NCIC) na wala sio DPP au IG ama Idara ya Kuchunguzi Uhalifu (DCI).

Jaji Ngaah aliagiza kesi hiyo ikabidhiwe DPP na washtakiwa wenzake IG ,DCI na NCIC katika muda wa siku saba.

DPP alikuwa ameagiza wanasiasa hao watatu wachunguzwe na kesi zao kuwasilishwa kortini mara moja.

Sheria Mtaani inasema sheria nambari 12 ya NCIC ya 2008 imeipa tume hiyo nguvu ya kuchunguza na kumfungulia mashtaka yeyote anayeeneza matamshi ya chuki.

  • Tags

You can share this post!

Ripoti yaanika jinsi makocha hutekeleza dhuluma za kimapenzi

Wabunge wataka CBC iondolewe, wasema ni ghali kwa wazazi na...

T L