Habari

Mahakama yatupa ombi la Aukot la kutaka jopokazi la BBI livunjwe

March 4th, 2020 1 min read

Na JOSEPH WANGUI

MAHAKAMA kuu Jumatano imetupa ombi la kiongozi wa Thirdway Alliance Kenya Ekuru Aukot la kutaka jopokazi la wataalamu wa mpango wa maridhiano (BBI) livunjwe.

Mahakama imesema Rais Uhuru Kenyatta akibuni jopokazi hilo dhamira yake kuu ilikuwa ni kuunganisha taifa na hivyo hakukuhitajika umma kuhusishwa.

Jaji John Mativo amesema mlalamishi alishindwa kuonyesha jinsi Rais alivyoonyesha ‘nia mbaya’ na namna ambavyo kubuniwa kwa jopokazi hilo kulivyokuwa ni kinyume cha sheria na ukiukaji wa Katiba.