Habari

Mahakama yazima agizo la Matiang'i kwamba raia wanne wa China wafurushwe

February 19th, 2020 1 min read

Na MWANDISHI WETU

MAHAKAMA imesitisha agizo la Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i la kuwarudisha nyumbani raia wanne wa China walioshtakiwa kumpiga Mkenya mkahawani jijini Nairobi.

Uamuzi umetolewa Jumatano na Jaji Luka Kimaru wa Mahakama Kuu.

Matiang’i alitoa agizo hilo wiki jana baada ya Hakimu Mwandamizi  wa Mahakama ya Milimani Bi Hellen Okwani aliyeruhusu maafisa wa polisi kumzuilia kuwazulia washukiwa hao wanne kwa siku 15 kukamilisha uchunguzi wa udhalimu wanaodaiwa kutekeleza na makosa yanayohusu ukiukaji wa sheria za usafiri na kazi.

Wanne hao ni Deng Hailan – anayedaiwa kumpiga Simon Osako Silo kwa kuchelewa kuingia kazini – akiwa na Chang Yueping, Ou Qiang and Yu Ling.

Kisa hicho kilifanyika katika mkahawa wa Chez Wou, Kileleshwa.