Habari

Mahindi: Wabunge kutoka North Rift wataka Kiunjuri ajiuzulu, atetea uamuzi wake

July 17th, 2019 1 min read

Na CHARLES WASONGA

WABUNGE kutoka North Rift wamemtaka Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri ajiuzulu kwa kuagiza mahindi kutoka nje.

Wabunge hao wamedai tayari Kiunjuri amelipa kampuni moja kwa jina Commodity House Ltd Sh1.8 b kuleta mahindi nchini.

Baadhi ya wabunge wa kutoka North Rift wawahutubia wanahabari Julai 17, 2019, katika majengo ya bunge la kitaifa. Picha/ Charles Wasonga

Na wakati huo huo, Kiunjuri aliyefika mbele ya Kamati ya Kilimo kuhusu Kilimo ametetea uamuzi wake wa kuagiza mahindi.

Waziri huyo amesema hakuna mahindi yatakayoagizwa kutoka North Rift mwaka 2019.

Badala yake, amesema magunia ‘machache’ yataagizwa kutoka Mataifa ya Afrika Mashariki, Ethiopia na mengine chini ya muungano wa kibiashara wa Comesa.

 

Taarifa kamili inatayarishwa…