Majaji 5 wazima mpango wa BBI

Majaji 5 wazima mpango wa BBI

Na RICHARD MUNGUTI

MCHAKATO wa ripoti ya maridhiano wa BBI jana ulipigwa breki na mahakama kuu ilipoizima Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuendeleza harakati za kufanikisha kufanyia katiba mabadiliko.

Majaji watano George Odunga, Profesa Joel Ngugi, Jairus Ngaah, Enock Chacha Mwita na Janet Mulwa walisitisha mchakato huo wa kufanyia katiba marekebisho hadi kesi saba zilizowasilishwa na makundi ya kutetea haki za binadamu isikizwe na kuamuliwa.

Hata hivyo majaji hao walisema ijapokuwa hawajazuia mabunge ya kaunti kujadili na kupitisha mswada uliowasilishwa na IEBC yanapasa kuelewa “maamuzi yao yanaweza kuharamishwa hatimaye kesi ya walalamishi hao saba ikiamuliwa hatimaye.”

  • Tags

You can share this post!

Taabani kwa kuuza vifaa feki vya kupima Ukimwi

Joho apuuza wanaomtaka adandie wilbaro