Kimataifa

Majambazi waitisha matiti 540 ya wanawake

May 23rd, 2018 1 min read

Na VALENTINE OBARA

JINJA, UGANDA

TAHARUKI imetanda katika Wilaya ya Jinja baada ya majambazi kutupa barua katika vijiji vitano wakitaka wakabidhiwe matiti 20 ya wanawake wakongwe, wake za watu 400 na wasichana 120 vijana.

Barua hizo ndogondogo zilizotuopwa katika vijiji vya Wakitaka, Kaitabawala, Namulesa, Lwanda na Sakabusolo vilivyo Kaunti Ndogo ya Mafubira, zilisema wasipokabidhiwa kile wanachotaka watashambulia wanakijiji.

Mwenyekiti wa Kaunti Ndogo ya Mafubira, Hamis Kiganyira, alisema majambazi hao pia wanataka wapewe pesa.

“Jumatatu nilikuwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Jinja katika mojawapo ya maeneo ambapo barua zilitupwa ili tutafute zilikotoka, lakini wakazi, hasa wanawake wakongwe wana hofu kubwa,” akasema.

Aliongeza kuwa wanakijiji walianza kushambuliwa hata kabla ya barua hizo kutupwa wikendi.