Habari Mseto

Majambazi wavamia wauzaji wa mifugo Bura

October 30th, 2020 1 min read

STEPHEN ODUOR NA FAUSTINE NGILA

Wafanyabiashara  sita walijeruhiwa Jumapili  asubuhi  kwenye mashambulizi yaliotokea  maeneo ya Bangale, Bura katika Kaunti ya  Tana River.

Kulingana na habari ya naibu kamishena wa kaunti hiyo Peter Munyoki wafanyabiashara hao walikuwa wakieleka soko ya mifugo walipovamiwana na wanaume watato waliokuwa wamejihami.

Bw Munyoki alisema kwamba wasahambulizi hao walidai  pesa kutoka kwaa wanabiashara hao na walipokataa wakavamiwwa vibaya sana.

Wanabiashra wawili walipigwa risasi ya mguuni huku wengine wanne wakipata majeraha kiasi.

“Inaonekana kwamba wavamizi hao walikuwa wanalenga  wafanyabiashara ambao walikuwa wakirudi kutoka sokoni kununua mifugo.”

Bw Munyoki alisema kwamba maafisa wa polisi wanfanya uchunguzi kuwaafuta washambulizi hao.