Habari Mseto

Majangili wapigwa dhamana ya Sh400,000

August 21st, 2020 1 min read

NA RICHARD MUNGUTI 

Washukiwa watutu wa uwindaji haramu walishtakiwa katika mahakama ya Kibera kwa kupatikana na pembe ya ndovu iliyo na uzito wa kilo nne.

Moctor Indwasi,Gladys Nyukuri na Achimidis Mbaluka walikana Ijumaa kortini Kibera walipatikana na pembe ya ndovu

Shtaka lilisema mnami Agosti 19 katika egesho ya Supa la Gallerie Langata Nairobi walikutwa na pembe ya ndovu iliyo na thamani ya Sh400000.

Watatu hao walikanusha shtaka na kuomba waachiliwe kwa dhamana.

Ombi la dhamana halikupingwa na kiongozi wa mashtaka George Obiri.

Kila mmoja aliagizwa na hakimu mkuu Abdulkadir Lorot awasilishe dhamana ya Sh400000 na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho.