Majangili wapigwa risasi na wanajeshi waliolenga wezi

Majangili wapigwa risasi na wanajeshi waliolenga wezi

Na AFP

Watu kadhaa walifariki katika mashambulio ya angani yaliyolenga kambi za wezi wa mifugo katika jimbo la Sokoto, kaskazini mwa Nigeria, duru zilisema Jumatatu jioni.

Mashambulio hayo yalitekelezwa na wanajeshi wa Nigeria katika kambi mbili katika wilaya ya Isa inayodhibitiwa na makundi mawili ya wahalifu- wamekuwa wakitekeleza mashambulio vijijini humo na kuiba mifugo.

Hii ilikuwa shambulio la kwanza aina hiyo kutekelezwa katika eneo hilo.“Wanajeshi waliendesha mashambulio ya angani katika vijiji vya Tsaika na Dangwandi ambako idadi kubwa ya majangili waliuawa,” afisa mmoja wa utawala katika wilaya ya Isa alisema.

“Sio rahisi kubaini idadi ya majangili waliouwa lakini idadi ni kubwa kwa sababu maiti za majangili hao zimetapakaa kote katika kambi hizo,” akaongeza afisa huyo ambaye aliomba jina lake libanwe

You can share this post!

Wahudumu ufuoni waanza kupewa chanjo

TAHARIRI: Vyama vikubwa visitumie hila kuzuia uhamaji

T L