Makala

Majani ya moringa na manufaa yake

June 4th, 2019 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MAJANI ya moringa nyana kiasi kikubwa cha madini kama sulphur na Vitamini E; vitu ambayo ni muhimu sana katika urembo.

Majani haya yana uwezo wa kuzifanya nywele ziwe nadhifu pamoja na kuzifanya zikue vizuri zaidi.

Pia yatafanya ngozi yako iwe ni ya kupendeza na kuiacha iking’aa pamoja na kuondoa chunusi kwenye ngozi.

Jinsi ya kutumia moringa kwenye ngozi

Unaweza kutengeneza facial toner kwa kuchemsha majani ya moringa kisha uyaweke kwenye jokovu tayari kwa matumizi. Fanya hivi mara kadhaa kwa wiki ili upate matokeo bora.

Jipake usoni kwa kutumia pamba safi na baada ya robo saa uoshe uso wako kwa maji ya kawaida.

Pia unaweza kutengeneza mask ya moringa.

Unahitaji

–      Unga wa majani ya moringa

–      Unga wa mdalasini

–      Maziwa

–      Asali

Cha kufanya

Changanya vitu hivi vyote vinavyohitajika kisha paka usoni. Baada ya robo saa, unaweza kunawa kwa maji ya kawaida.

Jinsi ya kutumia moringa kwenye nywele

Chemsha majani yako kisha yachuje na maji yake utumie kuoshea nywele zako.

Pia unaweza kutumia kabla ya kuosha nywele zako kwa shampoo. Ikiwa unataka kufanya hivi, ni bora uisage kwenye blenda kisha ukamue juisi yake na upake kwenye ngozi ya kichwa halafu uoshe baada ya nusu saa.

Mbali na hayo moringa pia ina manufaa kama vile;

Vitamini C – Kirutubishi hiki ni muhimu katika kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Calcium (madini chuma) – Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha pamoja na kujenga mifupa na meno mwilini.

Protini – Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga mwili na kuimarisha ngozi.

Vitamini A – Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha macho na kuongeza uwezo wa kuona.

Potassium – Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga na kuupatia mwili nguvu.