Maji ya Ziwa Victoria yasababisha kansa, watahadharisha wataalamu

Maji ya Ziwa Victoria yasababisha kansa, watahadharisha wataalamu

Na LEONARD ONYANGO

WATAALAMU sasa wanaonya kuwa watu wanaoishi karibu na Ziwa Victoria wako katika hatari kubwa ya kupatwa na maradhi ya kansa.

Utafiti uliofanywa na wataalamu kutoka Vyuo Vikuu vya Maseno, Moi na Masinde Muliro, ulibaini kuwa ‘uchafu’ wa rangi ya kijani ambao unaonekana ukielea juu ya maji ya Ziwa Victoria na vyanzo vinginevyo vya maji, unasababisha kansa.

Uchafu huo wa kijani unaojulikana kama ‘green algae’ ni bakteria wanaotoa sumu ya cyanotoxins ambayo husababisha kansa ya ini.Uchunguzi huo ulioanza tangu 2018, umebaini kuwa bakteria hao hatari pia wanapatikana katika visima na mito.

Prof David Onyango wa Chuo Kikuu cha Maseno anasema kuwa bakteria hao pia wanatoa sumu ambayo hutatiza ukuaji wa mtoto tumboni wakati wa ujauzito.Anaongeza kuwa wanapatikana katika baadhi ya maji ya chupa yanayouzwa madukani kwani hayasafishwi kwa kiwango kinachohitajika.

Prof Onyango anasema kuwa wengi wa watu wanaoishi karibu na ziwa hilo wanakunywa kiwango cha juu cha bakteria hao hivyo kujitia katika hatari ya kupatwa na saratani.Kadhalika wanaokunywa maji ya hayo moja kwa moja wako katika hatari kubwa ya kupatwa na matatizo ya tumbo kama vile kuhara.

 

You can share this post!

Wanajeshi wapindua serikali ya muda Sudan

Mwanamke ni shujaa

T L