Majonzi afisa akiua mpenziwe kisha kujiangamiza kwa risasi

Majonzi afisa akiua mpenziwe kisha kujiangamiza kwa risasi

Na OSBORN MANYENGO

POLISI katika kituo cha Kiungani, Trans-Nzoia wanaomboleza vifo vya maafisa wenzao wawili waliokuwa wanandoa.

Kamanda wa Polisi kaunti hiyo, Bi Jecinta Wesonga, alisema afisa wa cheo cha konstebo alimuua mpenziwe kabla ya kujimaliza kwa risasi.

Wawili hao walikuwa na mtoto wa kike wa umri wa mwaka mmoja.

Bi Wesonga aliwashauri maafisa wa polisi wawe wakitafuta ushauri nasaha ili kutatua matatizo yao wanapokumbwa na msongo wa mawazo, badala ya kujiua.

Mili ya hao imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Level 4 mjini Kitale huku uchunguzi ukiendelea kubaini haswa kilichosababisha wawili hao kujitoa uhai.

Huku pia kubaini ni nani alianza kufietulia rasasi na baadaye kujiua.

  • Tags

You can share this post!

Polisi wasaka walioua mtu kwenye baa

Ndoa mpya yatatiza mahesabu ya Ruto

T L