Majonzi mshambuliaji akiwaua wanafunzi 19

Majonzi mshambuliaji akiwaua wanafunzi 19

NA AFP

TEXAS, AMERIKA

WATU 21, wakiwemo wanafunzi 19, waliuawa Jumanne, baada ya mshambuliaji kufyatua risasi kiholela kwenye shule moja ya msingi mjini Uvalde katika jimbo la Texas, Amerika, huku Rais Joe Biden akitaka sheria kuhusu umiliki wa bunduki kurekebishwa.

Haya ni mauaji ya idadi kubwa zaidi ya watu tangu yale ya 2012, ambapo mshambuliaji aliwaua watoto 20 na wafanyakazi sita wa shule ya msingi mjini Sandy Hook.

Kijana wa umri wa miaka 18, aliivamia shule hiyo ya msingi katika mji mdogo wa Uvalde ulio karibu na mpaka wa Amerika na Mexico, na kuwamiminia risasi wanafunzi na wafanyakazi.

Shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 500, wengi wao wenye asili ya Kihispania na kutoka familia maskini.

Rais Biden alitumia hotuba hiyo kuhamasisha Waamerika kujitokeza na kupinga sheria inayoruhusu umiliki wa bunduki kiholela.

“Tumechoshwa na mauaji haya ambayo yamekuwa yakitekelezwa kiholela bila hatua kuchukuliwa. Sheria ya kudhibiti umiliki wa bunduki inafaa kuharakishwa,” akasema Rais Biden.

Gavana Greg Abbott wa jimbo la Texas alimtaja mshukiwa wa mauaji hayo kama Salvador Ramos, 18, raia wa Amerika.

Maafisa wa Idara ya Usalama wa Umma ya Texas walieleza kituo cha utangazaji cha CNN, kwamba kijana huyo anaaminika kuwa alimpiga risasi nyanya yake kwanza kabla ya kuelekea shuleni saa sita mchana, ambako aliingia akiwa na bunduki mbili na mavazi ya kujikinga risasi.

Ramos baadaye aliuawa na maafisa wa usalama.

  • Tags

You can share this post!

Kinyago yalipua Blue Boy huku Sharp Boys ikiangusha Young...

Ruto arushia wanawake chambo kwa ahadi ya kuwapa nusu ya...

T L