Habari Mseto

Majonzi mwili wa mfanyabiashara ukipatikana gesti

May 24th, 2024 1 min read

NA STEPHEN MUNYIRI

MWILI wa mfanyabiashara ambaye anashukiwa kujitoa uhai ulipatikana katika gesti mjini Karatina, Kaunti ya Nyeri, Jumatano.

Kamanda wa Polisi Mathira Mashariki, Bw Benjamin Boen, alisema kisa hicho kiliripotiwa na mhudumu wa gesti ya Parkway baada ya mteja huyo kukosa kuamka asubuhi.

“Bahasha iliyokuwa na namba za simu za kaka na dadake ilikuwa juu ya meza. Ndani ya gari lake kulikuwa na daftari iliyoeleza mali zake zote na maeneo ziliko,” alieleza Bw Boen.