Michezo

Makahaba 1,000 tayari kuandamana uchi iwapo Conte hatang’oka

April 30th, 2018 1 min read

Na MASHIRIKA

KATIKA jitihada za kushinikiza Chelsea kumwajiri kocha mpya, shabiki sugu wa kikosi hicho, Sophie Rose ameapa kuvua nguo na kusalia uchi wa mnyama kisha kushawishi makahaba 1,000 jijini London kutembea tuputupu iwapo bwanyenye Roman Abramovic hatamtimua mkufunzi Antonio Conte ugani Stamford Bridge mwishoni mwa msimu huu.

Baada ya kujichora makalioni kwa maandishi na nembo ya klabu yake wiki jana, Sophie amewataka mahawara kuonyeshana peupe miji yao kabla ya kuwaonjesha masogora wote wa Chelsea asali za mizinga yao mwishoni mwa mwezi huu katika hafla maalum atakayoingoza iwapo usimamizi wa ‘The Blues’ utaahidi kumfurusha Conte hata ikiwa atawavunia Kombe la FA.

Hadi kufikia sasa, dalili zote zinaashiria kwamba Chelsea watakosa kushiriki kipute cha Klabu Bingwa barani Ulaya (UEFA) msimu ujao na wako katika hatari ya kukamilisha kampeni za muhula huu bila taji lolote iwapo watazidiwa maarifa na Man-United katika fainali ya FA itakayowakutanisha ugani Wembley mnamo Mei 19, 2018.

Katika ishara zinazoonyesha kwamba mpango wa Sophie utafaulu, gazeti la The Sun limefichua kwamba makahaba, wanamitindo na wanenguaji viuno kadhaa wa kike jijini London tayari wameanza kutoa ahadi za ‘vitumbua’ vya bure katika sherehe zitakazowashuhudia wakipigana miereka na wanasoka wa Chelsea.

Sophie ambaye amewahi kuhusishwa na mazoea ya kuwatia kishawishini wanasoka wa haiba kubwa pamoja na watu maarufu katika tasnia mbalimbali, amekiri kuteswa na penzi alilonalo kwa fowadi wa zamani wa Arsenal, Olivier Giroud aliyejiunga na Chelsea mwanzoni mwa mwaka huu.

Kipusa huyo ambaye pia ni mwanahabari wa Chelsea Fan TV ana historia ndefu ya kujilegeza kimapenzi kwa wachezaji maarufu bila ya mahusiano yake ya siri kufichuka.

Hata hivyo, jaribio lake la hivi karibuni la kunyemelea na kuwania penzi la Giroud huenda likatia doa uhusiano wa mwanasoka huyo mzawa wa Ufaransa na mkewe Jennifer.