MAKALA MAALUM: Bidii ya bodaboda kujikwamua kutoka kwa lindi la umaskini

MAKALA MAALUM: Bidii ya bodaboda kujikwamua kutoka kwa lindi la umaskini

Na MAUREEN ONGALA

CHANGAMOTO za ukosefu wa ajira ambayo imechangia umaskini miongoni mwa vijana si sababu kuu ambayo ilisababisha vijana sita, wahudumu wa bodaboda kutoka mji wa Malindi kutafuta mbinu ya kipekee kujikimu kimaisha.

Licha ya wazo zuri la kuunda kikundi chao ili kuwa na uwezo wa kujiendeleza kiuchumi na kuinua maisha yao wahudumu hao wa bodaboda wanaopatikana katika kiingilio cha mji wa Malindi walipata pingamizi kutoka kwa wenzao ambao waliwapuuza na kusema mipango yao ilikuwa ni ndoto tu ambayo haingetimia kamwe.

Lakini bodaboda hao hawakufa moyo na mwaka wa 2012, Desemba waliunda kikundi walichokiita Malindi Entry Self Help Group ambapo walianzisha chama cha kuchanga Sh170 kila wiki.

Sh150 kutoka kwa kila mmoja wao ilipatiwa mmoja wa wanachama na Sh20 iliwekwa kama akiba ya kutumika wakati wa dharura.

Bidii ya bodaboda hao sita iliwatia tamaa wenzao ambao waliamua kujiunga na kikundi hicho kwa wingi na mnamo mwaka wa 2017 wanachama hao walibadilisha usajili wao kutoka kwa kikundi cha kujitegemea hadi Kikundi cha jamii ambacho kilijulikana kwa jina la Malindi Entry Development Group (MED GROUP) CBO.

Msemaji wa Malindi Entry Development Group Bw John Nzai alisimulia Taifa Leo juu ya safari yao ambayo ilikumbwa na milima na mabonde hadi sasa ambapo wanajihusisha katika bishara ya uchukuzi wa bodaboda na Tuktuk katika mji wa Malindi.

Bali na biashara ya uchukuzi wanachana mhao wanendeleza mradi ya elimu wa ‘Elimika Pwani’kuwasaidia wanafunzi kutoka familia maskini kwenda shule kwa kuwalipia karo,kuwanunulia sare za shule na mahitaji mengine ili kuhakikisha wanaendeleza masomo yao bila matatizo.

“Tulianza chama chetu na vikwazo na pingamizi kutoka kwa wanabodaboda wenzetu na ni sita tu ambayo tukukataa kushawishiwa na tukaamua kuanza safri yetu ya kupigana na unaskini,”akasema Nzai.

MSAADA

Takriban wanafunzi 30 wanaendelea kufaidika na msaada huo.

Balo na kuwa na chama chao cha kila wiki ambacho kilionyesha kusaidia wanachama hao kupata pesa za kushughukia baadhi ya matatizo madogomadogo Bw Nzai alisema kuwa walitumia nafasi yao kuandika mapendekezo na kuomba mkopo kutoka kwa hazina mbalimbali za pesa ya serikali ya taifa nay a Kaunti ya Kilifi.

Kikundi hicho kiliomba mkopo wake wa kwanza wa laki moja kutoka kwa hazina ya kuinua vijana ya Youth Fund mwaka 2013 na walafanikiwa kupata [pesa hizo mwaka wa 2014 mwaka mmoja baada ya kuwasilisha maombi yao.

“Tulikuwa tumekata matumaini ya kupata mkopo huo kwa minajili ya kuendeleza chama chetu lakini maombi yetu yalikubalika na tulitumia pesa hizo kunua pikipiki yetu ya kwanza,”akasena Nzai.

Msemaji huyo alizidi kueleza kuwa wanachama hao waliendelea kuchukua mikopo ya kibinafsi kutoka kwa chama chao kuendeleza bishara zao na pia kupata pesa za kulipia mkopo wao wa hazina ya vijana.

Walimaliza kulipa deni lao mwezi Juni 2015.

“Ilikuwa rahisi kwa wanachama kulipa mkopo huo kwa sababu masharti yake hayakuwa mahumu ikilinganishwa na taasisi zingine za fedha ambayo huwa changamoto kwa jamii kulipa madeni na hata wengi hunadiwa mali yao na kubaki maskini kushinda hali yao ya awali,”akasema.

Baada ya hapo vijana hao waliomba mkpo wa shilingi laki nne kutoka katika hazina ya Uwezo na pesa hizo walitumia kunua Tuktuk.

Waliomba tena mkopo katika hazina ya vijana na wakapewa laki mbili na walitumia pesa hizo kununua pikipiki yao ya pili.

Msemaji huyo alisema kuwa mafanikio yao ilichangiwa na wanachama anbao walijitolea kutimiza lengo lao kuangamiza umaskini na pia ndoto yao ya kutoa nafasi za ajira kwa vijana wenzao katika jamii.

“Mafanikio ya kikundi chetu ilikuwa dhihirisho kuwa vijana kutoka jamii ya Pwani wana uwezo wa kujiendeleza kiuchumi kama wenzao kutoka maeneo mengine ya nchi,”akasema Nzai.

Kikundi hicho kina wanachama 26, wanaume 14 na wanawake 12.

“Tunataka kuhakikisha kuwa tunapiga vita umaskini kwa huwawezesha vijana kujihusisha na miradi ya kuwaunua kiuchumi ambayo ni ya kudumu,” akasema.

Bidii ya wanachama hao kutafuta pesa ya kuinua kikundi chao ilizido kuendea baada ya wao kupokea mkopo mwingine wa nusu milioni kutoka katika hazina ya Vijana .

Walitumia pesa hizo kunua Tuktuk yao ya pili.

Kuwepo kwa wanawake katika kikundi hicho pia kiliwapa uwezo poa wa kuomba na kupata mkopo wa laki moja kutoka katika hazina ya serikali kuu ya kuwainua wanawake wa WEF(Women Enterprise Fund) .

Mnamo mwaka 2016 Bunge la Kaunti ya Kilifi ilipistisha sheria ya kuwepo kwa hazina ya Mbegu ambayo ingetoa mkopo kwa makundi ya wanamama,vijana na walemavu bila riba.

Malindi Entry Development Group (MED GROUP) walituma maombi yao kwa bodi ya Mbengu Fundu na wakapata mkopo wa lakini nne na pesa hizo walinunua Tuktuk ingine na kuongeza idadi kuwa tatu.

KOPESHA

Pia mradi wao amabao walikuwa wanaendeleza hapo awali wa kukopesha meza mezani kwa wanachama wake ulifaidika na granti ya shilingi lakini moja na hamsini kutoka kwa hazina na NG-Affirmative Action Fund (NGAAF).

Kwa sasa kikundi hicho kina tuktuk tatu,na pikipiki moja na pia shilingi lakini nne katika mfuko wao .

Katika lengo lao moja la kutoa nafasi za kazi kwa vijana ,wameajiri maderva kuendesha bodaboda na pikipiki hizo .

Ili kukuza wanachama wake,kikundi hicho kiliweka sheria kuwa pikipiki zote ambazo zitanunuliwa zitauziwa wanachama kwa bei ya chini badada ya mda ulio kubalika.

Kufikia sasa wanachama watatu tayari wanamiliki pikipiki. Na wanaendeleza bodaboda.

Bw Nzai alisema kuwa mojawapo ya lengo kuu ambalo lilichangia wanachama hao kutoka katika cha kujitegemea na kuunda kikundi cha jamii ni kutokana na ari ya kutaka kuona kuwa vijana wengi wanafaidika na pesa za serikali kwa njia tofauti.

Kufikia sasa makundi saba ya vijana yameundwa na kujiandikisha kufatia mafunzo na mwongozo wa Malindi Entry Development Group na tayari wanaendelea kutuma maombi ya kutaka mikopo ya kujiendeleza.

Bidii Kikundi hicho pia kilitambuliwa na United Nation Development Program (UNDP) kupitia almashauri ya kushughulikia ukame nchini (NDMA) na kutuzwa pikipiki tatu .

Hata hivyo Bw Nzai alisema kuwa kikundi hicho kinapitia baadhi ya changamoto kadhaa katika hali ya kutaka kujiendeleza ikiwemo pingamizi wakati wanapotaka kukutana na viongozi hasa wanasiasa ili kuweza kupata Baraka za kupanua biashara na kuendeleza malengo yao kupitia msaada kutoka kwa washikadau mbalimbali katika kaunti hiyo.

Hali mbovu za barabara wakati wa mvua na kiangazi imekuwa changamoto kwa wanabodaboda na pia tuktuk kwani huvunjika sehemu ambazo ni gharama ya juu kukarabati.

Pia hali mbovu uya usalama ambayo imechangia wahudumu wa bodaboda kuvamiwa na majambazi na kupokonywa pikipiki.

You can share this post!

Mitrovic wa Fulham awabeba Serbia katika ushindi wa 3-2...

TAHARIRI: Fedha: Kaunti zizingatie ushauri