• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:58 PM
Hofu huku idadi ya wanaume wanaokosa nguvu za kiume ikiongezeka

Hofu huku idadi ya wanaume wanaokosa nguvu za kiume ikiongezeka

Na CECIL ODONGO

WATAALAMU wa afya wamezua hofu kutokana na kuendelea kupanda kwa idadi ya wanaume tasa au wale ambao hawana nguvu za kiume.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mwanamume mmoja kati ya sita hana nguvu za kiume.

Kutokana na uhalisia huu, Wanasayansi 25 waliozamia utafiti wao walibaini kuwa wanaume wanastahili kumakinikia uchunguzi wa mapema kisha kukumbatia matibabu ili kutojipata kwenye hali ya kukosa nguvu za kiume.

Wataalamu hao wanasisitiza kuwa kutokana na ukosefu wa ujuzi kuhusu dalili za mapema za ukosefu wa nguvu za kiume, wanaume wengi hujipata wakiwa tasa bila kufahamu. Aidha juhudi kubwa zimekuwa zikielekezwa katika matibabu ya wanawake kuliko wanaume ambao ni tasa.

“Kuongezeka kwa wanaume ambao hawawezi kuzalisha hakuwezi kuhusishwa na jeni (genes) pekee bali pia hutokana na masuala ya kimazingira. Kati ya masuala hayo ni kupumua au kukumbana na kemikali zenye athari mbalimbali ambazo huvuruga homoni mwilini,” akaseema Sarah Kemmins Mwanasayansi kutoka Kituo cha Utafiti cha CRCHUM, Montreal Canada.

“Unene kupita kiasi, mtindo mbovu wa ulaji, kuvuta sigara na bangi pamoja na unywaji wa pombe kupita kiasi pia husababisha ukosefu wa nguvu za kiume. Kinachosikitisha ni kuwa wanaume wengi hawafahamu hivyo,” akaongeza.

Watafiti hao sasa wanapendekeza kuwa wanaume wawe wakichunguzwa hali yao kisha matibabu ya mapema kupendekezwa kusuluhisha hali hii.

Wengi wanaume ambao wana ukosefu wa mbegu za kiume hutabika sana baadhi wakiishia kupatwa na msongo wa mawazo kutokana na kejeli katika jamii.

Vilevile watafiti hao wanapendekeza mafunzo kwa wahudumu wa afya kuhusu uzazi wa wanaume na pia hamasisho ya mara kwa mara kuelimisha kuhusu tasa matibabu faafu.

  • Tags

You can share this post!

Raila afafanua kauli yake ya “Kalonzo Tosha”

Israeli yakanusha kusitisha mashambulio Ukanda wa Gaza

T L