• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 10:30 AM
Homoni za kiume huwa chache kwa wanaume wasiolala vya kutosha

Homoni za kiume huwa chache kwa wanaume wasiolala vya kutosha

NA CECIL ODONGO

WANASAYANSI wanashauri kuwa mtu mzima anastahili kulala kwa kati ya muda wa saa saba hadi saa tisa ili kutokuwa na tatizo la afya au kuyaepuka magonjwa mengi.

Wale ambao hulala kwa muda ambao ni chini wa huo au wa chini kabisa, wako katika hatari ya kuandamwa na maradhi mbalimbali sugu.

Kutokana na shughuli za kusaka riziki na kutimiza majukumu mbalimbali kuna wale ambao hukosa kulala ndani ya muda huo na wale ambao hulala kwa muda mdogo mno.

Pia kuna wale ambao hutumia mihadarati kama miraa ambayo huwahini usingizi wao.

Katika suala hatari ambalo huenda likawatishia wanaume wasiolala na kuwapa kiwewe, wanasayansi wamebaini kuwa kukosa usingizi wa kutosha husababisha homoni chache za kiume ipungue na pia mbegu zao kiume huathirika kwa kushuka ubora.

Watafiti kutoka Marekani walizama na kuthibitisha kuwa ukosefu wa usingizi hupunguza ukubwa wa testerone ambayo kibayolojia ina homoni za kiume zinazochangia kuongeza hamu ya ngono.

Kwa kawaida korodani huongezeka ukubwa wakati ambapo mwanaume hulala na huanza kupungua wakati wamefikisha umri wa miaka 40. Hii ina maana kuwa wanaume ambao wametimu umri huo na pia hukosa usingizi wa kutosha, wataathirika zaidi na kuwa na korodani ndogo.

Pia, imebainika kuwa wakati ambapo homoni za kiume hupungua kwenye korodani, homoni inayoitwa Cortisol ambayo huzuia mwanaume kulala, husambaa sana mwilini na kufanya akose usingizi wakati mwingi.

Kinaya ni kuwa mwanaume akila akilala vizuri basi homoni za kiume huzalishwa kwa wingi na kuimarisha afya yake kisha humsaidia wakati wa mapenzi.

  • Tags

You can share this post!

Uhispania Marathon: Cheptegei wa Uganda anyemelea rekodi ya...

Miili iliyokuwa inatafutwa baada ya gari kusombwa na maji...

T L