• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 6:55 AM
Akilimali: Mfumaji zulia Samuel Ruiru

Akilimali: Mfumaji zulia Samuel Ruiru

Na PATRICK KILAVUKA

Aliyesema ukuona vyaelea jua vimeundwa hakukosea kwani, mfumaji Samuel Ruiru anaamini sindano ya kufuma, gunia la mfuko na uzi tu vyaweza kubadilisha maisha ya mfumaji.

Mfumaji Ruiru anasema alifanya kazi ya kuajiriwa kabla kuwa na ari ya kufanya kazi ya mkono ya kufuma mwaka 2017 ambayo imebadilisha maisha yake! Ukiona kazi ya ufumaji ya zulia amefanya mfumaji huyo inavyopendeza, utaamini kwamba kizuri kweli chajiuza.

Kwa kufanya mauzo akitembelea sehemu mbalimbali akiwauzia na kuwahamasisha wanunuzi/ wateja jinsi ya kufuma, amefua dafu kupata mauzo kibao kwani anaweza kuuza zaidi ya mikeka tatu kwa siku ambazo anaziuza zaidi 600-800. Mbali na kuuza sindano za kufuma kubwa Sh350 na ndogo Sh200 ambazo zinaenda kama keko moto.

Si hayo tu, zulia kubwa zaidi inauzwa kuanzia Sh10,000. Mfumaji Ruiru huvumisha biashara yake kupitia kutembelea mji na mitaa mbalimbali zikiwemo Nakuru, Nairobi, Limuru, Kiambu, mtaa wa kangemi na kadhalika. Isitoshe, anaiuza na kupata oda kupitia mtandao Decorative mats.

Kufunza na kuelekeza wateja wake anapowauzia na kuwatumia video ambazo amezirekodi wakati anapounda, kumeimarisha uteja kwani anaamini mteja anafaa kuelewa vyema kitu anachouziwa kumpa uwezo wakitumia na kukitunza.

Mfumaji zulia au mikeka Samuel Ruiru akifuma huku zilizomalizika zikiwa kwenye maonyesho akiziuza pia wakati alipotembelea mtaa wa Kangemi kufanya mauzo na kuhamasisha wateja…Picha/PATRICK KILAVUKA

Anasema ni rahisi kufuma mikeka hii almradi ufuate utaratibu za kufuma. Kwa kuchora mtindo unataka kuunda kwenye zulia, unaweza kuufuma kwa kutumia uzi za rangi mbalimbali kuitia nakshi au ulimbwende.

Isitoshe, anasema rangi za mkeka unaounda yategemea ni wapi utatumia mkeka iwe ndani ya nyumba au kwenye mlango au veranda. Nje au veranda anadokeza kuwa yafaa utumie rangi ambazo si angavu sana na zisizoonyesha uchafu kwa urahisi.

Hata hivyo, anadokeza zulia hii, ni rahisi kuitunza kwani ikichafuka, unaweza tu kuiosha na kuuanika ikauke na kuurudi kutandika. Gunia inayotumiwa kuiunda ni ile inayoweza kuwaoshwa pasi na shida yoyote kwani, ni ile hailoeki au kuiharibiki kwa urahisi ikishafuma.

Fauka na shindano na uzi kuwa zile zipatikanao,” afichua mfumaji Ruiru ambaye alifundishwa kazi hii na mfumaji Njenga ambaye pia anaunda sindano anazotumia.Anaarifu kwamba kufanya mazoezi ya kila mara kwaimarisha kazi ya kufuma.

Changamoto ilikuwa wakati wa mwanzoni kuiunda. Lakini sasa kazi imekuwa rahisi kila uchao na ana uwezo wa kuunda zulia hata zaidi ya mbili kwa siku. Ujumbe wake ni kwamba, milango ya kazi za mkono imo katika ari ya kujituma na laiti vijana wangejua kutumia talanta zao nafasi za ajira zingekuwa wazi kuliko zile za maofisi ambazo huadimika kama wali wadaku.

Mfumaji zulia au mikeka Samuel Ruiru akifuma huku zilizomalizika zikiwa kwenye maonyesho akiziuza pia wakati alipotembelea mtaa wa Kangemi kufanya mauzo na kuhamasisha wateja…Picha/PATRICK KILAVUKA

You can share this post!

Wandani wa Joho sasa tishio kwa ODM Pwani

MC Jessy ajiunga na UDA

T L