• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 2:24 PM
Akothee ajitambulisha kama ‘singo matha’ licha ya kufunga ndoa

Akothee ajitambulisha kama ‘singo matha’ licha ya kufunga ndoa

Na MWANDISHI WETU

MWANAMUZIKI Esther Akoth almaarufu Akothee bado anajitambulisha kama rais wa wazazi wa pekee wa kike (single mothers) licha ya kuolewa.

Akothee aliyefunga ndoa Aprili 2023 na hata kushauriwa kuondoa jina hilo anapojitambulisha bado anasisitiza kuwa yeye ndiye rais wa kundi hilo.

Kwenye mazungumzo yake na jirani yake kwenye ndege alipokuwa akisafiri kuenda Uswizi, Akothee alisema kuwa anaenda kusherehekea fungate yake.

“Unafanya nini ili kujimudu kimaisha?” jirani huyo akamuuliza.

“Mimi ni mama wa pekee kwa watoto wangu watano na ninaelekea kuona kama nitaweza kupata wengine wawili na bwana yangu,” Akothee akaeleza.

“Kwa hivyo unafanya kazi tu nyumbani,” akaendelea jirani.  “La! mimi ni rais wa wazazi wa pekee wa kike,” akamjibu.

Akothee alijibatiza rais wa wazazi wa pekee wa kike na kwenye kurasa zake za kijamii aliwapa wosia kina mama hao.

Mwanamuziki huyo aliwashauri wazazi hao kujipenda na kutopigana na wazazi wa kiume wa watoto wao.

Kwa kujitumia kama mfano, Akothee aliwaonya kina mama hao dhidi ya kuwakataza watoto wao kutangamana na baba zao akisema kuwa watoto wanapokua watawatafuta kwani damu ni nzito kuliko maji.

Baada ya ndoa yake, mwanahabari Betty Kyallo aliapa kuchukua nafasi hiyo ya rais wa wazazi wa pekee wa kike.

“Ametoa msongamano. Alikuwa rais wa wazazi wa pekee wa kike sasa inaonekana mimi sasa ndiye nitakuwa next,” Kyallo akasema kwenye harusi.

Kuolewa kwa Akothee kulifanya wengi kuzungumza kuhusu wadhifa huo aliojibandika huku hata mhubiri Ezekiel Odero akiwashauri wote ‘waliokuwa wakifanya kazi’ na Akothee katika wadhifa huo kuolewa.

“Hata yule binti anaitwa Akothee aliyekuwa anaitwa rais wa wazazi wa pekee wa kike ameolewa, wewe pia uolewe kwa jina la Yesu Kristo. Kama rais ameolewa, mawaziri na makatibu wakuu (CAS) pamoja na wafanyakazi wote wa serikali wote waolewe. Niliona nikafurahi nikasema ikiwa rais wa wazazi wa pekee wa kike ameolewa basi wale wote wanaojiita hivyo pia wapate roho ya ndoa,” akasema

  • Tags

You can share this post!

Rais atelekeza ahadi baada ya kutua ikulu

Polisi mchoraji ahimiza wenzake watumie talanta kuzima...

T L